29 Aprili 2025 - 19:51
Source: IQNA
Waandamanaji  wanaunga mkono Palestina London wapinga Israel kuuziwa silaha

Mbio za Marathon za London zilikumbwa na vurugu baada ya waandamanaji kuitaka serikali ya Uingereza kuweka vikwazo kamili vya biashara dhidi ya Israel.

Waandamanaji walisisitiza hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza na kuikosoa serikali ya Uingereza kwa kuunga mkono utawala wa Israel  unaoendeleza vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.

Wanachama wawili wa Youth Demand, kikundi kinachoongozwa na vijana cha upinzani wa kiraia nchini Uingereza, waliruka vizuizi karibu na Daraja la Tower na kumwaga rangi nyekundu ya unga mbele ya wakimbiaji. 

Waandamanaji hao walikuwa wamevaa fulana zenye ujumbe wa ‘Acheni Kufadhili Israel’ na walikamatwa na polisi. 

Taarifa kutoka Youth Demand kwenye X ilisoma kuwa Gaza "inakaribia kumaliza chakula" na kwamba "Kufadhili mauaji ya kimbari ni kuvuka mstari." 

Polisi ya Metropolitan ya Uingereza ilisema kwenye X kwamba wafanyakazi wa marathon waliingilia kati kuwaondoa waandamanaji kutoka kwenye njia ya mbio na mbio hizo ziliendelea bila kuzuiwa. Polisi waliwakamata waandamanaji kwa tuhuma za kusababisha usumbufu wa umma, na wanashikiliwa korokoroni. 

Kabla ya maandamano, Willow Holland, mwenye umri wa miaka 18 kutoka Bristol, alisema alichukua hatua hiyo kwa sababu mbinu nyingine, kama maandamano na mikutano ya hadhara, zilishindwa kusimamisha mauaji ya kimbari huko Gaza, ambako Israel imewaua zaidi ya watu 52,000 tangu Oktoba 2023. “Faida haipaswi kupewa kipaumbele zaidi ya utu wa kawaida,” alisema katika taarifa iliyotolewa na kikundi hicho. 

Kikundi hicho pia kiliikosoa serikali ya Uingereza, kikisema jeshi limeendesha zaidi ya safari 500 za ndege za kijasusi juu ya Gaza tangu Desemba 2023, jambo lililoongeza hofu ya kushirikiana katika mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita wa Israel.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha